Maelfu ya raia wa kigeni wameondoka Afrika Kusini kufuatia vitisho vilivyotolewa na makundi yanayopinga wahamiaji, yaliyotaka wageni wasio na vibali kuondoka nchini kabla ya tarehe 30 Juni 2026.
Katika miezi ya hivi karibuni, maandamano dhidi ya wahamiaji yameongezeka katika miji kadhaa, huku watu watatu, akiwemo raia mmoja wa Malawi na wawili wa Msumbiji, wakipoteza maisha katika vurugu zilizotokea katika majimbo ya KwaZulu-Natal na Western Cape.
Serikali ya Afrika Kusini ilizindua operesheni maalumu ya polisi ili kuzuia vurugu zaidi, huku ikitangaza hatua za kuimarisha usalama wa mipaka na kukabiliana na wahamiaji wasiokuwa na nyaraka halali.
Kutokana na hofu ya mashambulizi, mamia ya wahamiaji walikusanyika nje ya ofisi za Idara ya Mambo ya Ndani mjini Durban wakisubiri kurejeshwa katika nchi zao. Baadhi yao walilazimika kuacha nyumba na shughuli zao za kujipatia kipato baada ya maandamano dhidi ya wageni kugeuka vurugu.
Taarifa ya BBC