Mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati akamatwa Molo

Eric Asande Albert mwenye umri wa miaka 45, alipatikana na bangi yenye thamani ya shilingi milioni moja nyumbani kwake, kwenye msako huo.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mshukiwa wa mihadarati akamatwa Molo.

Maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) wamemkamata mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati katika eneo la Munju, Molo, kaunti ya Nakuru.

Eric Asande Albert mwenye umri wa miaka 45, alipatikana na bangi yenye thamani ya shilingi milioni moja nyumbani kwake, kwenye msako huo.

Kwenye ukurasa wa X, DCI ilisema maafisa wa kitengo cha kukabiliana na mihadarati (ANU), walitekeleza msako wa kijasusi na kupata gunia lililojaa bangi, mifuko ya kubebab mizigo yenye uzani wa kilo 55, na gunia nusu lililokuwa bangi.

“Maafisa wa polisi walipekua moja ya vyumba vyake na kupata bidhaa hiyo haramu,” ilisema DCI.

Kulingana na maafisa hao, bangi hiyo inazuiliwa na itatumika kama ushahidi, huku Albert akizuiliwa katika kituo cha polisi cha Molo akisubiri kufikishwa mahakamani.

TAGGED:
Share This Article