Rais Ruto apongeza timu ya Kenya iliyoshiriki michezo ya Commonwealth

Kwenye mashindano hayo, Kenya ilimaliza ya 12 baada ya kupata nishani 12, dhahabu 3, Fedha 4 na shaba 5.

Tom Mathinji
1 Min Read
Kenya ilipata medali 12 kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola.

Rais William Ruto ameipongeza tmu ya Kenya iliyoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyoandaliwa Jijini Glasgow Scotland,

Kwenye mashindano hayo, Kenya ilimaliza ya 12 baada ya kupata nishani 12, dhahabu 3, Fedha 4 na shaba 5.

“Tunawapongeza wanariadha wetu walioshinda dhahabu Edmund Serem (mita 3,000m kuruka kidimbwi cha maji), Mathew Kipchumba Kipsang (Mita 5,000), na Faith Cherotich (Mita 3,000 kuruka kidimbwi cha maji),” aliwapongeza Rais Ruto.

Kwenye mbio hizo wanariadha waliopata fedha ni pamoja na Stephen Ndangiri Kihu (Mita 10,000 kutembea), Simon Kiprop Koech (Mita 3,000 kuruka kidimbwi cha maji), Diana Wanza (Mita 10,000), na  Lilian Odira (Mita 800.

Walioshinda shaba ni Bravo Leonard Kipkemoi Bett (Mita 3,000m kuruka kidimbwi cha maji), Wyclife Kinyamal (Mita 800), Timothy Cheruiyot (Maili moja), Irene Jepkemboi (Javelin), na Joshua Amunga Mboya (Kuinua uzani wa kilo 60).

Tunawaenzi kwa matokeo bora na shukran sana kwa kuipeperusha bendeera ya Kenya,” alisema Rais Ruto.

Share This Article