Edmund Serem alikata kiu ya Wakenya aliponyakua dhahabu ya kwanza katika makala ya 23 ya michezo ya Jumuia ya Madola inayoendelea mjini Glascow ,Scotland Jumatatu usiku.
Serem ambaye ni bingwa wa Dunia kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20 mwaka 2024 alitwaa uongozi katika mzunguko wa mwisho na kuibuka mshindi kwa kutumia dakika 8 sekunde 18.23,huku Wakenya akifagia nishani zote tatu.
Simon Koech alishinda fedha kwa dakika 8 sekunde 18.59,wakati Leonard Bett ,akishinda shaba kwa dakika 8 sekunde 21.63.
Awali Diana Wanza alipoteza rada katika mzunguko wa mwisho na kuridhia nishani ya fedha kwenye fainali ya mita 10,000.
Wanza alikalimisha mbio hizo za mizunguko 24 kwa dakika 31 sekunde 50. 13, huku Mnyarwanda Florence Niyonkuru akishinda shaba.
Kenya imezoa medali 1 ya dhahabu,2 za fedha na shaba mbili kufukia sasa.