Msimu wa mwaka 2025/2026 wa Ligi Kuu Kenya ulikamilika Jumapili Mei 31, kwa mechi za raundi ya 34,huku Gor Mahia wakitawazwa mabingwa kwa mara ya 22.
Pia ilikuwa mara ya kwanza kwa Gor, kunyakua taji hiyo tangu msimu wa mwaka 2023/2024, kabla ya kupokonywa na Police FC msimu jana.
Kwa jumla Gor walizoa alama 69,wakishinda 20,kutoka sare tisa na kupigwa mara 5.
AFC Leopards walimaliza wa pili kwa pointi 64 nao Police FC, wakaambulia nafasi ya tatu kwa alama 55,mbili juu ya Nairobi United, iliyochukua nafasi ya nne, wakati Shabana FC wakifunga tano bora kwa pointi 52.
Timu za Kariobangi Sharks,Bidco United na Sofapaka zilishuka ngazi.