Tanzania ukipenda Twiga Stars, walisajili ushindi wa kwanza katika historia ya kombe la mataifa ya Afrika WAFCON baada ya kuwanyuka mabingwa wa mwaka 2022, Afrika Kusini, mabao 2-1, Jumatatu jioni katika mchuano wa kundi B.
Majirani Tanzania walichukua uongozi kunako dakika ya 37, kupitia kwa bao la Diana Msewa, lakini Banyana Banyana wakakomboa dakika ya 2 ya muda wa ziada kipindi cha kwanza kupitia kwa Bambanani Mbane.
Zikisalia dakika tatu kipenga cha mwisho kipulizwe Hasnath Ubamba, aliwanyanyua mashabiki wa Tanzania, alipopiga bao la pili na ushindi,ukiwa ushindi wa kwanza kwa Twiga Stars wanaoshiriki WAFCON ya tatu.
Tanzania sasa wanahitaji ushindi dhidi ya Burkina Faso, Ijumaa hii ili kufuzu kwa robo fainali kwa mara ya kwanza katika historia.