Timu ya Kenya ya wanawake ya soka ,Harambee Starlets itafungua kampeni yake katika makala ya 14 ya kipute cha Kombe la mataifa ya Afrika (WAFCON),Jumapili usiku dhidi wenyeji Morocco kuanzia saa tano usiku.
Kenya chini ya Kocha Beldine Odemba, inarejea katika mashindano hayo kwa mara ya kwanza baada ya mwongo mmoja.
Upande wao Morocco maaraufu kama Atlas Lioness,wataandaa kipute hicho kwa mara ya tatu mtawalia,wakimaliza nafasi ya pili katika makala ya mwaka 2022 na 2024.

Mechi hiyo itatanguliwa na pambano la ufunguzi kundini A,baina ya Algeria na Senegal, kuanzia saa mbili usiku.
Kando na kuwania Kombe la Afrika ,timu nne bora zitafuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Brazil.
Jumla ya mataifa 16 yanashiriki kindumbwendumbwe hicho kutoka kwa timu 12 zilizoshiriki makala ya mwaka 2024.
Mechi zote za kipute hicho zitarushwa mubashara na runinga ya taifa KBC,Channel 1.