Chama cha DP chataka wahuni kukomeshwa

Martin Mwanje
1 Min Read
Justin Muturi - Kiongozi wa chama cha DP

Chama cha Democratic Party of Kenya (DP) kimelalamikia vitendo vya uhuni vinavyoendelea kushuhudiwa nchini na kutaka jinamizi hilo kupigwa breki mapema kabla maji hayajazidi unga. 

Kiongozi wa chama hicho Justin Muturi amelalamikia hatua ya wahuni kuwashambulia wanahabari wakati wa uchaguzi mdogo ulioandaliwa katika eneo bunge la Ol Kalou siku chache zilizopita akitaja kitendo hicho kuwa tishio kwa uanahabari.

“Mashambulizi hayo ya kikatili dhidi ya wanahabari wakati wa uchaguzi mdogo wa hivi karibuni yanatisha. Ripoti za kuchukuliwa kwa vifaa vyao vya kazi na kuharibiwa kwa magari ya wanahabari, ni ishara ya jaribio la wazi la kuzuia uanahabari huru, kuficha maovu na kutishia vyombo vya habari,” alisema Muturi ambaye pia ni Waziri wa zamani wa Utumishi wa Umma.

“Kwa hivyo tunatoa wito kwa washikadau katika anga ya demokrasia – ikiwa ni pamoja na vyama vya kisiasa, mashirika ya kijamii, ya kidini, tume za kikatiba, washirika wa maendeleo na Wakenya wapenda amani kuitisha mazungumzo ya kitaifa ya dharura juu ya kulinda mustakabali wa demokrasia nchini Kenya.”

Share This Article