serikali yaonya wahuni, yaapa kuwachukulia hatua kali

Martin Mwanje
1 Min Read
Isaac Mwaura - Msemaji wa serikali

Mtu yeyote anayejihusisha na vitendo vya kihuni atachukuliwa hatua kali ya kisheria punde ushahidi dhidi yake utakapobainika. 

Msemaji wa serikali Isaac Mwaura ameonya kuwa serikali haitavumilia kukithiri kwa vitendo vya kihuni nchini.

“Msimamo wa serikali ni kwaamba hakuna njia yoyote ambayo tunaweza kuvumulia uhuni. Huo siyo msimamo wa serikali. Tunakashifu vitendo kama hivyo, na hata ipo ripoti ambayo tumeipata ni kwamba sasa watu wamejipanga, wamekuwa organized, mpaka wanarecruit wengine, online. Siyo vizuri hata kidogo,” alisema Mwaura wakati akiwahutubia wanahabari leo Jumatatu.

Mjini Busia, mbunge wa Teso Kaskazini Oku Kaunya amelaani vitendo vinavyoongezeka vya uhuni nchini na kuwataka wanasiasa wenzake kukoma kuwatumia vijana kuzua vurugu ili kuendeleza maslahi yao ya kibinafsi.

Chama cha DP kupitia kwa kiongozi wake Justin Muturi pia kimelaani kuongezeka kwa vitendo vya kihuni na kutoa wito wa kuandaliwa kwa mazungumzo ya kitaifa ili kutafuta njia mwafaka za kukabiliana na jinamizi hilo.

Share This Article