Wakenya watakiwa kutokubali kugawanywa na uchaguzi

Rais William Ruto amesema daima kutakuwa na maisha baada ya uchaguzi na kuwasihi Wakenya kudumisha amani nyakati zote. 

Martin Mwanje
1 Min Read
Mpiga kura akishughulikiwa na maafisa wa IEBC wakati wa uchaguzi mdogo wa Ol Kalou

Rais William Ruto ametoa wito kwa Wakenya kutoruhusu uchaguzi kutishia umoja wa taifa. 

Ruto amesema daima kutakuwa na maisha baada ya uchaguzi na kuwasihi Wakenya kudumisha amani nyakati zote.

Amesema punde uchaguzi unapomalizika, Wakenya wanapaswa kukumbuka kuwa Kenya ni nchi ya wote.

“Uchaguzi si kitu cha kufa kupona. Kutakuwa na Kenya baada ya uchaguzi na tunapaswa kuishi pamoja kwa amani kama ndugu na dada wa taifa moja,” alishauri Rais.

Kadhalika amewataka Wakenya kutokubali kugawanywa kwa misingi ya kikabila.

Akizungumza alipokutana na viongozi wa mashinani kutoka kaunti ya Bungoma katika Ikulu ya Nairobi leo Ijumaa, Ruto amesema kuna ya viongozi kuelekeza shabaha yao kwa kuwatumikia raia.

Amesema viongozi, akiwemo mbunge mpya wa Ol Kalou Sammy Kamau Ngotho, watahukumiwa kutokana na rekodi yao ya maendeleo.

“Kitu cha msingi zaidi ni kuhakikisha maisha ya wanaotupigia kura yanaboreka,” aliongeza Ruto.

Alisema Kenya inaweza kubadilishwa tu kupitia mipango na miradi ya maendeleo.

 

Share This Article