Wafanyabiashara katika mtaa wa Greatwall Gardens, Athi River katika kaunti ya Machakos wameandamana kulalamikia ongezeko la vibanda visivyostahili katika mtaa huo na kutatizika kwa biashara halali zinazolipa ushuru.
Wakiongozwa na Fred Muka, wanadai serikali ya kaunti ya Machakos imekuwa ikishirikiana na wafanyabiashara hao kuwaruhusu kujenga vibanda nje ya maduka ya mtaa huo.
Wanalalama kwamba hatua ambayi imetatiza biashara halali na kukosa wateja ilhali wana mzigo wa ushuru.
Serikali ya kaunti ya Machakos kupitia Raphael Kithala ambaye ni afisa wa utawala wa eneo la Athi River imeelezea kupokea malalamishi na kuahidi kusuluhisha mzozo huo.
Taarifa ya Jonathan Musau