Shirikisho la Soka Duniani, FIFA limezindua mpira mahususi utakaotumika kwa mechi za nusu fainali na fainali ya Kombe la Dunia mwaka huu.
Mpira huo aina ya Trionda ni tofauti na ile ya awali ambayo itatumika hadi kufikia robo fainali kwani una rangi ya dhahabu.
Mpira wa Trionda ambao umekuwa ukitumika unajumuisha rangi nyekundu, samawati, kijani na nyeupe.
Nusu fainali ya Jumanne usiku itakuwa kati ya Uhispania na Ufaransa katika uchanjaa wa Dallas nchini Marekani.
Nusu fainali ya pili itakuwa kati ya mabingwa watetezi Argentina dhidi Uingereza Jumatano, Julai 15 katika kiwara cha Atlanta.
Fainali itakasatwa Julai 19 ugani New York/New Jersey.