Mashirika ya ndege ya Ulaya yaonywa dhidi ya safari katika mataifa ya Ghuba

radiotaifa
1 Min Read

Shirika la Usalama wa Anga la Umoja wa Ulaya (EASA) linaonya mashirika ya ndege dhidi ya kusafiri kwenye anga ya Bahrain, Kuwait, Qatar, UAE, na juu ya maji ya Ghuba ya Oman.

Linasema “matukio ya kijeshi yasiyotabirika, pamoja na uwezekano wa matumizi ya makombora, ndege zisizo na rubani, ndege za kivita na mifumo ya ulinzi wa anga” ndani ya eneo hilo ni “hatari” kwa safari za ndege.

EASA inasema ushauri huu utaendelea kudumishwa hadi tarehe 29 Julai, ikiongeza kuwa itafuatilia hali hiyo kwa karibu.

Taarifa ya BBC

Share This Article