Timu ya taifa ya ya Kenya – Harambee Stars, itarejea uwanjani Marrakech nchini Morocco, kukabiliana na Chad, katika mchuano wa pili wa kimataifa wa kirafiki.
Timu hizo zilitoka sare tasa zilipokutana Juni saba katika uwanja huo.
Kenya ni ya 111 katika msimamo wa FIFA, huku Chad ikishikilia nambari 177.
Pambano hilo litang’oa nanga saa kumi na mbili jioni.
Harambee Stars inatumia mchuano huo kujiandaa kwa Makala ya nane ya fainali za Kombe la nane la CHAN.