Spika Wetang’ula awapongeza wanafunzi walioshinda tuzo za kimataifa

Wanafunzi wa Kenya walishindana katika vitengo vinne vya network, computing, cloud na uvumbuzi wa AI .

Dismas Otuke
1 Min Read

Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, amewapongeza wanafunzi wa Kenya walioshinda tuzo za kimataifa katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Wetang’ula amesema haya Jumatatu alipopokea ujumbe wa wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Kenya waliopokea tuzo za Huawei zilizoandaliwa nchini Uchina.

Wanafunzi wa Kenya walishindana katika vitengo vinne vya network, computing, cloud na uvumbuzi wa AI .

“Nachukua fursa hii kuwapongeza kwa maarifa yenu maridhawa na kuipeperusha bendera ya taifa ipasavyo.” akasema Spika Wetang’ula.

Wanafunzi hao waliandamana na Naibu Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Huawei Kenya, Steven Zhang; Mkurugenzi wa shirika la Talent Ecosystem, Michael Kamau; Mkurugenzi wa masuala ya serikali na afisa wa ushirikiano wa umma, Bi Khadija Ahmed; na Mkurugenzi wa masuala ya umma, Yuta Leng.

Website |  + posts
Share This Article