Polisi jana wamewanasa washukiwa watatu wa ulanguzi wa mihadarati mtaani Kasarani katika kaunti ya Nairobi.
Polisi walifanya oparesheni hiyo na kunasa kilo 50 za bangi na misokoto mingine 810 ya bangi.
Washukiwa hao wamewekwa kwenye korokoro ya polisi wakisubiri kufikishwa mahakamani.
Huduma ya kitaifa ya Polisi imekariri kujitolea kumaliza ulanguzi wa mihadarati nchini na kuwataka wananchi kusaidia kwenye kampeni hiyo.