Makasisi wa Kanisa Katoliki hapa nchini, wamelaani mauaji ya kutatanisha ya Albert Ojwang’ yanayodaiwa kutokea katika kituo cha polisi cha Central, Jijini Nairobi.
Kupitia kwa taarifa, Baraza Kuu la Makasisi wa Kanisa Katoliki (KCCB), lilitaja mauaji ya Ojwang kuwa sio tu mkasa kwa familia, lakini ni kidonda kwa taifa nzima kwa jumla.
“Kifo chake sio pigo tu kwa familia, lakini kidonda chenye uchungu kwa taifa hili na kumbukumbu la dharura ya uwajibikaji katika mfumo wa sheria,” lilisema Baraza hilo.
Aidha Makasisi hao, walituma rambirambi kwa familia na marafiki wa marehemu Ojwang’, huku wakiungana na wake ya wengine kutaka haki na ukweli kutendewa familia ya marehemu.
Viongozi hao wa kanisa katoliki waliunga mkono hatua ya Inspekta Mkuu wa Polisi Douglas Kanja ya kuwasimamisha kazi kwa mua maafisa waliokuwa zamuni, ili kutoa fursa kwa uchunguzi huru na wa haki kutekelezwa.
Wakati huo huo walitoa wito kwa wananchi kuwa watulivu, waombezi na kujizuia na visa vyovyote vinavyochochea ghasia na migawanyiko.