14 wakamatwa kuhusiana na vurugu maeneo ya Kisumu na Nyandarua

Martin Mwanje
1 Min Read
Wanaoshukiwa kuchochea vurugu walikamatwa wakiwa na silaha mbalimbali

Jumla ya watu 14 wamekamatwa kuhusiana na vurugu zilizoshuhudiwa katika maeneo ya Kisumu na Nyahururu mwishoni mwa wiki iliyopita.

Huduma ya Taifa ya Polisi, NPS inasema 14 hao wanaoshukiwa kuchochea vurugu hizo watafikishwa mahakamani leo Jumatatu.

“NPS haitavumilia vurugu, uhuni na usumbufu wowote wa amani ya umma,” ilisema Huduma hiyo kwenye taarifa.

“Tunasalia imara katika wajibu wetu wa kudumisha sheria na usalama. Hebu ifahamike vyema: wale wanaochagua vurugu watakabiliwa vilivyo kisheria.”

Upinzani umeinyoshea Huduma ya Taifa ya Polisi kidole cha lawama kwa kuzembea katika kuwawajibisha watu wanaojihusisha na vitendo vya uhuni nchini.

 

Share This Article