Shirikisho la soka Duniani linatafakari kuongeza idadi ya timu zitakazoshiriki fainali za Kombe la Dunia kuanzia mwaka 2030 kutoka 48 hadi 64.
Rais wa FIFA Gianni Infantino, amesema kuongeza timu kutatoa fursa kwa mataifa zaidi kupata fursa ya kushiriki kipute hicho.
Katika makala yanayoendelea nchini Marekani,Canada na Mexico,timu 48, zinashiriki kutoka idadi ya awali ya timu 32,na Afrika iliwakilishwa na mataifa 10 kwa mara ya kwanza.
Endapo idadi hiyo itaongezwa huenda pia Afrika iwakilishwe na timu zaidi ya tisa zilizofuzu moja kwa moja kwa makala ya mwaka huu.
Kipute cha Kombe la Dunia mwaka 2030, kitaandaliwa kwa pamoja na mataifa ya Ureno,Morocco na Uhispania.