Mabingwa watetezi Argentina,watakumbana na Uingereza, katika nusu fainali ya Kombe la Dunia Jumatano ijayo Julai 15.
Argentina imekuwa ya mwisho kufuzu kwa nusu fainali kufuatia ushindi wa mabao 3-1, kupitia muda wa ziada dhidi ya Uswizi katika robo fainali ya mwisho iliyotitigwa kiwarani Kansas,Marekani.
Alexis Mac Allister, aliwaweka Argentina, kifua mbele kunako dakika ya 10 na kuongoza hadi mapumzikoni.
Uswizi walibadili mchezo kipindi cha pili na Ricardo Rodríguez, alimdokolea pasi Dan Ndoye, katika dakika ya 67 na kutikisa nyavu kwa bao la kusawazisha na dakika 90 kuishia nguvu sawa.
Julian Alvarez alipachika bao la uongozi kwa Argentina dakika ya 112 ,na kisha Lautaro Martinez akazima matumaini ya Uswizi kurejea mchezoni kwa bao la tatu dakika 121.
Argentina watashuka uwanjani Atlanta ,Jumatano ijayo kwa nusu fainali ya pili dhidi ya Uingereza iliyowalemea Norway 2-1, katika muda wa ziada kwenye robo fainali ya kwanza Jumamosi usikui.