The Red Devils ya Ubelgiji walitoka nyuma mabao 2-0 na kuwashinda Teranga Lions kutoka Senegal mabao 3-2 katika mechi ya raundi ya 32 iliyochezwa Jumatano usiku uwanjani Seattle nchini Marekani.
Senegal walitawala mechi hiyo kutoka mwanzo na kutwaa uongozi dakika ya 25 kupitia kwa Habib Diarra na kudumu hadi mapumzikoni.
Simba wa Teranga waliendeleza na mashambulizi na umiliki mkubwa wa mpira na ilichukua tu dakika sita za kipindi cha pili kabla ya Ismaila Sarr kutanua uongozi kwa goli la pili.
Akidhani amesehinda, kocha wa Senegal alifanya mabadiliko ya kuwaondoa Papa Gueye, Ilman Ndiaye na Habib Diarra ndani ya muda wa dakika saba, na athari yake ikawapa Ubelgiji nguvu mpya.
Romelu Lukaku na Youri Tielmans waliwanyanyua mashabiki wa Mashetani Wekundu, kwa kupachika goli moja kila mmoja ndani ya kipindi cha sekunde 61.
Mchuano uliishia muda wa ziada na katika dakika ya 120, nguvu mpya Lamine Camara alimwangusha Tielmans kaktika kijisanduku na wakapata penalti iliyofungwa na Tielmans.