Wajumbe wa Marekani na Iran wameshiriki mikutano tofauti na wapatanishi jijini Doha nchini Qatar katika hatua ambayo imesifiwa na Rais wa Marekani Donald Trump.
Akizungumza na wanahabari jimboni Marylanda nchini Marekani jana Jumatano, Trump alisema mazungumzo hayo yanapiga hatua na kwamba “wanaelewana vizuri mno.”
“Kwa kadiri mambo yanavyoenda, kuondokana kabisa na silaha za nyuklia nchini Iran kunaendelea vizuri. Na wamekuwa na mikutano mizuri, na tutaona.”
Matamshi yake yanakuja wakati ambapo maafisa wa Marekani wamekutana na Waziri Mkuu wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani mjini Doha.
Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance amesema walijadili juu ya Mlango Bahari wa Hormuz.