Wanafunzi 8 wa Utumishi Girls wafikishwa mahakamani, wakana mashtaka

Wanafunzi hao walikana mashtaka 16 ya mauaji yanayowakabili walipofikishwa mbele ya Jaji Diana Kavedza wa Mahakama Kuu ya Kibera.

Martin Mwanje
1 Min Read
Wanafunzi 8 wa shule ya Utumishi Girls Academy walipofikishwa katika Mahakama Kuu ya Kibera Julai 1, 2026

Wanafunzi 8 wa shule ya Utumishi Girls Academy mjini Gilgil, kaunti ya Nakuru wanaotuhumiwa kwa kusababisha mkasa wa moto Mei 28 mwaka huu wamefikishwa mahakamani na kukana mashtaka dhidi yao.

Wanafunzi hao walikana mashtaka 16 ya mauaji yanayowakabili walipofikishwa mbele ya Jaji Diana Kavedza wa Mahakama Kuu ya Kibera.

Kesi dhidi yao ilitatajwa rasmi leo baada ya wao kufanyiwa uchunguzi wa kiakili katika Hospitali ya Akili ya Mathare.

Kiini cha kesi dhidi yao ni kufariki kwa wanafunzi 16 kwenye mkasa wa moto uliotokea katika shule ya Utumishi Girls Academy Mei 28.

Wanafunzi wengine 79 walijeruhiwa kwenye mkasa huo.

Uchunguzi wa awali ulibaini bweni la shule hiyo lilitetekezwa kimakusudi na kusababisha maafa hayo, mkasa unaoshukiwa kusababishwa na wanafunzi hao.

Serikali imeapa kuwachukulia hatua kali wanafunzi watakaopatikana wakijiusisha katika uovu kama huo siku zijazo.

Share This Article