Kocha wa Czechia, Miroslav Koubek abwaga manyanga

Jamhuri ya Czechia ilimaliza ya mwisho kundini A, kwa alama moja pekee baada ya kushindwa na Korea Kusini na Mexico.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kocha wa Czechia Miroslav Koubek amejiuzulu siku kadhaa baada ya timu yake kubanduliwa nje ya patashika inayoendelea ya Kombe la Dunia.

Jamhuri ya Czechia ilimaliza ya mwisho kundini A kwa alama moja pekee baada ya kushindwa na Korea Kusini na Mexico.

Koubek aliye na umri wa miaka 74 alitwaa mikoba ya ukufunzi kabla ya mechi za mchujo kufuzu kwa Kombe la Dunia na akawaongoza kusajili ushindi dhidi ya Ireland na Denmark na kufuzu kwa Kombe la Dunia baada ya subira ya miaka 20.

Haya yanajiri huku kocha wa Ujerumani Julian Naglesman akisimama kidete kuwa kamwe hatajiuzulu licha ya mabingwa hao mara nne wa Dunia kutemwa nje jana usiku na Paraguay.

Ni mara ya tatu mtawalia kwa Ujerumani kutimuliwa nje ya Kombe la Dunia mapema baada ya kufurushwa katika hatua za mwanzo mwanzo miaka ya 2018 na 2022.

Share This Article