Messi avunja rekodi huku Argentina ikifuzu kwa hatua ya 32 bora

Messi amevunja rekodi ya mfungaji bora katika Kombe la Dunia akiwa na jumla ya magoli 18, akivunja rekodi ya Miroslav Klose wa Ujerumani, aliyekuwa kuwa anashikilia rekodi ya awali ya mabao 16.

Dismas Otuke
1 Min Read

Nahodha wa Argentina Lionel Messi ameiongoza timu yake kufuzu kwa awamu ya 32 bora baada ya kufunga mabao 2 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Austria katika mechi ya kundi J uwanjani Dallas Jumatatu usiku.

Messi, licha ya kupoteza penalti ya dakika ya 9, alipachika bao la kwanza kunako dakika ya 38, akiunganisha krosi ya Facundo Medina.

Kipindi cha pili, mabingwa watetezi Argentina waliendeleza shinikizo na licha ya Austria kujaribu kwa udi na ambari kusawazisha, mabeki walikaa ange.

Hata hivyo, Austria wakati wakiendeleza mashambulizi walipatwa kwa shambulizi la kushtukiza ambapo Messi alicheka na nyavu dakika ya 95 .

Argentina imekuwa timu ya nne kutinga raundi ya 32 bora ikiwa na alama 6 kundini J, na kujihakikishia nafasi ya kwanza.

Argentina inajiunga na Marekani, Mexico na Ujerumani katika awamu ya mwondoano.

Messi amevunja rekodi ya mfungaji bora katika Kombe la Dunia akiwa na jumla ya magoli 18, akivunja rekodi ya Miroslav Klose wa Ujerumani, aliyekuwa kuwa anashikilia rekodi ya awali ya mabao 16.

Aidha, Messi aliye na umri wa miaka 38, ndiye mfungaji bora kwa mabao 5.

Share This Article