Chama kinachoongozwa na Waziri Mkuu Abiy Ahmed kimeibuka mshindi wa uchaguzi mkuu wa Ethiopia ulioandaliwa mapema mwezi huu.
Chama cha The Prosperity kilipata viti 438 kati ya viti 501 na sasa kinatarajiwa kubuni serikali ijayo huku Abiy akitarajiwa kuapishwa kwa muhula mwingine kuanzia mwezi Oktoba.
Hata hivyo, uchaguzi huo haukufanyika katika eneo la Tigray na baadhi ya maeneo ya Amhara.
Ushindi huo ni afueni kwa wafuasi wa Abiy ambao wanaamini kuwa ataendelea kuimarisha uchumi wa taifa hilo.
Katika eneo la Tigray, waaandalizi wa uchaguzi huo walitaja ukosefu wa usalama kuwa chanzo cha kukosa kuandaa uchaguzi huku eneo la Amhara likidaiwa kukaliwa na wanamgambo wa Fano.
Abiy, mwenye umri wa miaka 49, aliingia madarakani mwaka 2018.