Israel na Lebanon zimetia saini makubaliano ya kimkakati Jijini Washington, baada ya siku kadhaa za mazungumzo yaliyoongozwa na Marekani.
Makubaliano hayo yanalenga kusitisha vita kati ya Israel na kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, amesema makubaliano hayo yataweka mfumo wa amani na usalama wa kudumu.
Balozi wa Lebanon Nada Moawad na mwenzake wa Israel Yechiel Leiter, walitia saini makubaliano hayo nchini Marekani, huku maelezo machache yakitolewa kuhusu mkataba huo.
Haya yanajiri huku mapigano madogo yakiendelea kati ya vikosi vya Israeli na Hezbollah kusini mwa Lebanon, licha ya kuwepo mkataba wa kusitishwa kwa mapigano.
Hata hivyo, Hezbollah haikushiriki katika makubaliano ya Ijumaa, na haijulikani kama itakubali kuwaondoa wapiganaji wake kutoka eneo la Litani Kusini lililoko kusini mwa Lebanon.
Mzozo kati ya Israel na Hezbollah ulizuka wakati wapiganaji wa kundi hilo walishabulia Israel Machi 2, 2026, siku chache baada ya Marekani kuishambulia Iran.