Halaand awanyofoa Simba wa Teranga huku radi ikisitisha mechi ya Ufaransa

Mechi hiyo ilisitishwa kwa saa mbili kuanzia dakika za mwisho za kipindi cha kwanza, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha ikiambatana na radi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Erling Haalanda alicheka na nyavu mara mbili na kuwasaidi Norway kuwalabua Senegal mabao 3-2 katika mechi ya kundi I mapema Jumanne katika uwanja wa Metlife mjini New York, New Jersey.

Holmgren Pedersen alikuwa amepachika bao la kwanza mwishoni mwa kipindi cha kwanza kabla ya Halaand kutanua uongozi dakika tatu ndani ya kipindi cha pili.

Ismaila Sarr alikomboa goli moja kwa Simba wa Teranga katika dakika ya 53 lakini Halaand akaongeza la tatu kwa Norway dakika tano baadaye.

Sarr aliwatoa kijasho Norway baada ya kutikisa nyavu katika dakika ya 93, lakini Norway wakakaza kamba na kuibuka kidedea kwa magoli 3-2.

Ufaransa walikuwa wa kwanza kufuzu kwa awamu ya 32 bora kutoka kundi hilo la I baada ya kuwatitiga Iraq mabao 3-0 katika uwanja wa Philadelphia nchini Mareakni.

Kylian Mbappe alipachika mawili naye Ousman Dembele akaongeza moja kuwahakikishia Le Blues ushindi huo.

Mechi hiyo ilisitishwa kwa saa mbili kuanzia dakika za mwisho za kipindi cha kwanza, kufuatia mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha ikiambatana na radi.

Kama tahadhari, mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa nchini Marekani iliamrisha kusitishwa kwa mechi hiyo kwa dakika 30 kila wakati radi inapopiga kutoka umbali wa kati ya kilomita 12 hadi 16 kutoka uwanjani.

Share This Article