ODM yamvua Sifuna wadhifa wa Katibu Mkuu

Hatua hiyo ya Jumatatu,  ilitekelezwa na Kamati Kuu ya Kitaifa ya chama hicho (NEC).

Tom Mathinji
2 Min Read
Edwin Sifuna - avuliwa wadhifa wa Katibu Mkuu wa ODM.

Chama cha Orange Democratic Movement (ODM), kimemuondoa Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna wadhifa wa  Katibu Mkuu.

Hatua hiyo ya Jumatatu,  ilitekelezwa na Kamati Kuu ya Kitaifa ya chama hicho (NEC).

Kupitia kwa taarifa baada ya mkutano wa NEC, Kaimu Katibu Mkuu wa ODM Catherine Omanyo, alisema hatua hiyo iliafikiwa na kamati ya kutatua mizozo ya ndani ya chama  (IDRC) ambayo ilikubaliana kwa kauli moja kumtimua Sifuna afisini.

“Baada ya kuangalia ripoti hiyo na mapendekezo ya IDRC chini ya sehemu ya  74(2)  ya katiba ya chama hicho, NEC iliamua kwa kauli moja kutekeleza mapendekezo hayo na kumuondoa afisni Seneta Edwin Watenya Sifuna.  Kuanzia sasa Seneta Sifuna sio katibu Mkuu wa chama cha ODM,” alisema Omanyo.

Kulingana na chama  hicho, hatua hiyo ilifuata kikamilifu mchakato wa nidhamu wa chama hicho, baada ya Sifuna kupinga hatua ya ODM kwenye jopo la kutatua mizozo ya vyama vya kisiasa (PPDT).

Hata hivyo, ODM ilishikilia kuwa mchakato wake ulizingatia kikamilifu katiba ya chama hicho.

Kwenye uamuzi uliotolewa Juni 18, 2026, jopo hilo lilisema hakukuwa na ushahidi kwamba Sifuna alifahamishwa mienendo yake ingejadiliwa kwenye mkutano wa NEC, uliomfurusha afisni.

Jopo hilo chini ya mwenyekiti Gad Gathu, liliikosoa ODM kwa kumuondoa Sifuna wadhifani, bila kumpoa fursa ya kujitetea dhidi ya madai aliyolimbikiziwa.

Share This Article