Idadi ndogo ya mashabiki wa Cape Verde walijimwaya uwanjani Miami Jumapili usiku kuishabikia timu hiyo ilipotoka sare na Uruguay katika mechi ya kundi H,mapema Jumatatu.
Miongoni mwa mashabiki waliokuwa uwanjani Miami ni Ana Candida Evora, mamake mlinda lango Josimar José Évora Dias,amaarufu Vozinha,aliyepata umaarufu mkubwa baada ya kupangua matobwe saba katika mechi dhidi ya Uhispania na kulazimisha sare tasa katika mechi ya ufunguzi.
Bi, Evora alikosa kusafiri kuenda Marekani kushuhudia mechi ya kwanza dhidi Uhispania baada ya kukosa Viza.
Kipa Vozinha alipata umaarufu sana huku idadi ya wafuasi wake kwenye mtandao wa Instagram ikiongezeka kutoka 50,000, hadi zaidi ya milioni 15, baada ya mechi yao na Uhispania.
“Sikua hata na Pasipoti ,ni mara yangu ya kwanza nimesafiri nje ya cape Verde.Nimefurahia kuwa hapa sina maneno ya kuelezea .Kijana wangu amepitia mengi.”akasema Evora
Rais wa Marekani Donald Trump aliamrisha Evora, asafirishwe hadi Marekani kumtazama mwanawe akicheza.
Cape Verde itachuana na Saudi Arabia katika mechi ya mwisho ya kundi hilo mapema Jumamosi hii ,mchuano utakaobaini endapo watafuzu kwa hatua ya 32 bora au la.