FIFA World Cup: Ghana wang’aa dhidi ya Panama

Kipute hicho cha 23 kinaingia mechi za mzunguko wa pili hatua ya makundi leo usiku.

Dismas Otuke
1 Min Read

Black Stars ya Ghana walihitaji bao la Caleb Yirenkyi kunako dakika ya 95 kusajili ushindi dhidi ya Panama katika mchuano wa kundi L uliosakatwa usiku wa manane kiwarani BMO mjini Toronto, Canada.

Ghana wanaofunzwa na kocha mkongwe Carlos Queiroz, walisumbuliwa na Panama walioonekana kutafuta pointi ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia, lakini kosa la dakika za mwisho likawapa Ghana fursa ya kupachika bao.

Black Stars wanaongoza kundi hilo pamoja na Uingereza kwa pointi 3, huku Panama na Croatia wakiwa bila alama.

Mechi ya mwisho ilishuhudia pia Colombia wakiwalabua limbukeni Uzbekistan magoli 3-1 katika kundi K mapema Alhamisi uwanjani Arzteca mjini Mexico.

Colombia wanaongoza kundi K kwa alama 3 wakifuatwa na DRC na Ureno kwa alama 1 kila moja.

Kipute hicho cha 23 kinaingia mechi za mzunguko wa pili hatua ya makundi leo usiku.

Share This Article