Thomas Partey apoteza rufaa ya kunyimwa viza ya Canada

Aidha, litakuwa pigo kuu kwa Ghana kukosa huduma za mwanandinga huyo katika fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Ndoto ya kiungo wa Ghana Thomas Partey kushiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka huu imegonga mwamba, baada ya mahakama ya rufaa kutupilia mbali kesi aliyowasilisha mchezaji huyo kupinga kunyimwa cheti cha usafari kuingia nchini Canaada.

Partey ambaye zamani aliichezea klabu ya Arsenal alizuiliwa kuingia nchini Canada kushiriki Kombe la Dunia na kumlazimu kukata rufaa kupitia kwa wakili wake.

Masaibu hayo yana maana kuwa kiungo huyo atakosa mechi ya leo usiku baina ya Ghana na Panama ya kundi L, na pia nyingine za makundi dhidi ya Uingereza na Croatia.

Partey anakabiliwa na madai kadhaa ya ubakaji wakati akicheza soka ya kulipwa na Arsenal.

Aidha, litakuwa pigo kuu kwa Ghana kukosa huduma za mwanandinga huyo katika fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.

Share This Article