Nahodha Lionel Messi aliwaongoza mabingwa watetezi Argentina kuwakomoa Algeria mabao 3-0 katika mechi ya kundi J mapema leo Jumatano katika uwanja wa Arrowhead mjini Kansas nchini Marekani.
Messi alipachika mabao hayo kunako dakika za 17, 60 na 76 huku ikiwa hat trick ya kwanza kwa nyota huyo katika Kombe la Dunia na pia ya kwanza kwenye fainali za mwaka huu.
Ushinde wa Algeria maarufu kama Dessert Foxes uliendeleza rekodi yao mbovu, wakishinda mechi moja pekee kati ya 10 walizocheza tangu wafuzu kwa mara ya kwanza mwaka 1982.

Messi, aliye na umri wa miaka 38, kwa sasa amemfikia Miroslav Klose wa Ujerumani kuwa mfungaji bora wa Kombe la Dunia kwa magoli 16.
Katika mchuano mwingine, Norway iliwatitiga Iraq mabao 4-1 katika kundi I, Erling Halaand akitikiza nyavu mara mbili.
Halaand anajiunga na Kylian Mbappe wa Ufaransa, Kai Hervetz kutoka Ujerumani, Elijah Henry Just wa New Zealand,
Folarin Balogun wa Marekani na Yasin Ayari wa Uswidi kama wachezaji waliopachika mabao 2 kila mmoja.
Austria imewazabua limbukeni Iraq mabao 3-1 katika pambano jingine la kundi J mapema leo.