Raia wa Uganda akamtwa kwa ulanguzi wa mihadarati Naivasha

Tom Mathinji
1 Min Read
Raia wa Uganda akamatwa kwa ulanguzi wa mihadarati.

Raia wa Uganda amekamatwa kwenye barabara kuu ya Maai Mahiu- Naivasha, katika operesheni iliyowalenga washukiwa wa ulanguzi wa mihadarati.

Baada ya kupashwa habari, maafisa kutoka kitengo cha kukabiliana na mihadarti (ANU), na wale wa kitencho cha kukabiliana na uhalifu wa kupangwa  (TOCU),  walietekeleza operesheni katika eneo la Longonot kwenye barabara hiyo, ambapo walifanikiwa kupata mihadarati hiyo.

Aidha, maafisa hao walipata mifuko mitatu ya bangi iliyokuwa imewekwa kwenye sanduku la vifaa za gari lenye nambari za usajili  UBN 042.

Kupitia kwa ukurasa wa X, Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI, ilisema mshukiwa huyo Daniel Mudubo mwenye umri wa miaka 40 alikamatwa papo hapo.

“Gari hilo pamoja na bangi iliyonaswa zilipelekwa hadi kituo cha polisi cha Muthaiga, huku uchunguzi ukiendelea” ilisema taarifa hiyo ya DCI.

Share This Article