Mwanamuziki wa Marekani Oliver Tree afariki kwenye ajali ya helikopta

Oliver alikuwa miongoni mwa watu sita waliofariki baada ya helikopta mbili kugongana zikiwa angani.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwanamuziki wa Marekani Oliver Tree afariki kwenye ajali ya helikopta.

Mwanamuziki wa Marekani Oliver Tree amefariki kwenye ajali ya helikopta iliyotokea Jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil.

Oliver alikuwa miongoni mwa watu sita waliofariki baada ya helikopta mbili kugongana zikiwa angani.

Tree mwenye umri wa miaka 32, alikuwa mwenye ziara ya ulimwengu wakati ajali hiyo ilipotokea, huku moja ya helikopta ikionekana ikianguka kutoka angani hadi kwenye sehemu ya kuuza  magari na kusababisha takriban magari 20 kuteketea.

Maafisa nchini Brazil wamsema uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Oliver Tree Nickell, alizaliwa California mwaka 1993 na alipata umaarufu kwa mara ya kwanza mwaka 2016 baada ya kuenea kwenye mitandao ya kijamii.

Share This Article