Limbukeni Curacao wapigwa kitutu na Ujerumani

Ujerumani watarejea uwanjani kwa mkwangurano wa pili dhidi ya Ivory Coast Juni 20, huku Ecuador wakikabiliana na Curacao siku moja baadaye.

Dismas Otuke
1 Min Read

Limbukeni Curacao waliambulia kichapo cha mabao 7-1 katika pambano la kundi E kuwania Kombe la Dunia Jumapili jioni katika uwanja wa Houston nchini Marekani.

Mabingwa wa Dunia mara nne walianza vyema mechi hiyo huku Felix Nmecha akifungua karamu ya mabao kunako dakika ya sita pekee.

Livano Comenencia alikomboa bao hilo kwa Curacao dakika 15 baadaye huku Nico Schlotterbeck akitanua uongozi wa Wajerumani naye Kai Havertz akaongeza la tatu mwishoni mwa kipindi cha kwanza kupitia penalti.

Wajerumani waliendelea kutia fora walikoachia kuelekea mapumziko wakicheka na nyavu mara nne.

Jamal Musialana, Nathaniel Brown, Dennis Undav na Havertz waliongeza bao moja kila mmoja.

Ujerumani watarejea  uwanjani kwa mkwangurano wa pili dhidi ya Ivory Coast Juni 20, huku Ecuador wakikabiliana na Curacao siku moja baadaye.

Share This Article