Pigo kwa Morocco,wachezaji Aguerd na Ezzalzouliwakiondolewa kikosini

Simba wa Atlas waliocheza hadi nusu fainali ya mwaka 2022, wamo kundi moja la C pamoja na Brazil,Haiti na Scotland.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Morocco Atlas Lions imepatwa na pigo baada ya wachezaji wake nyota wakiwemo beki Nayef Aguerd, na Wing’a Abde Ezzalzouli,kuondolewa kikosini kutokana na majeraha.

Taarifa hizo za kutamausha zinajiri kabla ya Simba wa Atlas kuchuana na mabingwa mara tano wa Dunia Brazil, katika mchuano wa ufunguzi wa kundi C Jumamosi usiku.

Kulingana na shirikisho la soka nchini Morocco, wachezaji hao wawili hawatacheza Kombe la Dunia mwaka huu.

Aguerd, ambaye ni beki tegemeo wa Morocco na klabu ya Olympic Marseille, amekuwa akikabiliwa na jerahana kwa miezi kadhaa tangu ajeruhiwe mwezi Machi.

Ezzalzouli ambaye ni Wing’a wa klabu ya  Real Betis, alipata jeraha la goti akicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Norway.

Difenda Marwane Saadane na wing’a Amine Sbai, waliokuwa kwa orodha ya wachezaji wa ziada wameitwa kutwaa nafasi hizo.

Simba wa Atlas waliocheza hadi nusu fainali ya mwaka 2022, wamo kundi moja la C pamoja na Brazil,Haiti na Scotland.

Share This Article