Tanzania na Singapore zakubali kushirikiana

Pia Singapore ilikubali kufungua ubalozi wake jijini Dar es Salaam.

Dismas Otuke
1 Min Read

Tanzania na Singapore zimetia saini mikataba kadhaa ya kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali.

Mikataba hiyo ilisainiwa wakati wa ziara ya siku tatu ya Rais wa Singapore Tharman Shanmugaratnam nchini Tanzania.

Shanmugaratnam na mwenyeji wake Samia Suluhu Hassan, walisaini mikataba ya kuimarisha ushirikiano wa ukuaji wa kiuchumi, makuzi ya kidijitali, kilimo, afya na ukuzaji maarifa.

Pia Singapore ilikubali kufungua ubalozi wake jijini Dar es Salaam.

Rais Shanmuratnam alizuru Tanzania kwa mwaliko wa Rais Samia.

Share This Article