Kenya na Norway zimesaini mikataba ya ushirikiano katika kuleta amani na utatuzi wa mizozo, kupunguza uchafuzi wa mazingira na matumizi ya nishati safi.
Aidha, nchi hizo mbili zimejadiliana na kuafikiana kuimarisha ushirikiano wa kibiashara, uwekezaji na kukabilaina na mabadiliko ya tabia nchi.
Rais William Ruto anayeongoza ujumbe wa Kenya, alishuhudia kutiwa saini kwa mikaba hiyo siku ya Jumanne pamoja na Waziri Mkuu wa Norway Jonas Gahr Støre.