Mabadiliko serikalini: Ololtuaa kusimamia elimu, Bitok apelekwa utalii

Mabadiliko hayo yameanza kutekelezwa mara moja.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto siku ya Jumanne amefanya mabadiliko ya Makatibu wa Wizara mbili.

Kwenye mabadiliko hayo, Ruto amemhamisha John Ololtuaa kutoka Wizara ya Utalii hadi ile ya Elimu ya Msingi kuchukua nafasi ya Julius Bitok.

Naye Bitok amehamishiwa Wizara ya Utalii kutoka ile ya Elimu ya Msingi kurithi wadhifa wa Ololtuaa.

Mabadiliko hayo yameanza kutekelezwa mara moja.

Uteuzi wa Ololtuaa kusimamia elimu ya msingi unajiri wakati ambapo elimu ya sekondari inakabiliwa na changamoto kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa za migomo ya wanafunzi na kusababisha shule kadhaa kufungwa.

Haya yanajiri takriban majuma mawili baada ya wanafunzi tisa kushukiwa kuchoma bweni la shule ya Utumishi Girls Academy katika kaunti ya Nakuru na kusababisha vifo vya wenzao 16.

Haijulikani ikiwa changamoto hizo zimekuwa chimbuko la Bitok kuhamishwa kutoka wizara hiyo.

Awali, Katibu huyo mpya wa Wizara ya Utalii alihudumu katika Idara ya Uhamiaji kabla mahali pake kuchukuliwa na Dkt. Belio Kipsang.

 

Share This Article