Wasanii Shakira na Burna Boy, wameongezwa katika orodha ya waimbaji watakaotumbuiza katika sherehe za kufungua fainali za Kombe la Dunia mjini Mexico Juni 11.
Wawili hao wataimba kibao chao cha Dai Dai ambao ni wimbo rasmi wa kipute cha mwaka huu.
Sherehe za kufungua kombe la Dunia zitaanza dakika 90, kabla ya mechi ya ufunguzi .
Shakira na Burna Boy wanajiunga na wasanii wengine watakaotumbuiza wakiwemo; Alejandro Fernández, Belinda, Danny Ocean, J Balvin, Lila Downs, Los Ángeles Azules, Maná, Shakira na Tyla.
Wimbo wa Dai Dai, unalanga kuchangisha dola laki moja za Marekani sawa na Shilingi bilioni 12.9 za Kenya, kugharamia masomo ya watoto na mafunzo ya soka kwa watoto kote duniani.