Harambee Starlets watua Zambia kujipiga msasa

Kenya itakuwa ikicheza WAFCON kwa mara ya pili tangu mwaka 2016.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Kenya-Harambee Starlets, imewasili mjini Lusaka,Zambia Jumatano jioni tayari kwa mechi mbili za kirafiki kujiandaa kwa fainali za WAFCON.

Starlets wanaoongozwa na kocha Beldine Odemb,a watapiga mechi ya kwanza Juni 6 uwanjani Levy Mwanawasa, kabla ya kumaliza udhia na wenyeji Zambia siku tatu baadaye.

Kenya watatumia mechi hizo kujiandaa kwa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika- WAFCON, kati ya Julai 26 hadi Agosti 16.

Kenya itakuwa ikicheza WAFCON kwa mara ya pili tangu mwaka 2016.

Share This Article