Kenya yahimiza ushirikiano dhabiti wa kiteknolojia kati ya Afrika na Korea

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi.

Kenya imetoa wito wa ushirikiano dhabiti katika ya Afrika na korea, ili kufanikisha ukuaji endelevu na ushughulikiaji wa pamoja wa changamoto ibuka duniani.

Akizungumza kwenye mkutano wa Mawaziri wa Afrika na Korea Jijini Seoul, Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi,alidokeza kuwa ushirikiano ulioimarishwa kati ya Afrika na Korea, ni muhimu katika kuchochea ubadilishanaji wa teknolojia,maarifa na  ukuaji wa viwanda.

Mudavadi aliangazia majukumu ya taasisi kama vile Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA) na benki ya Korea ya Exim, katika kuunga mkono mageuzi ya kiuchumi ya Kenya, ubadilishanji wa teknolojia na ukuaji wa sekta ya kibinafsi.

“Afrika na Korea lazima ziimarishe ushirikiano ambao unainua ufanisi wa pamoja, ukuaji endelevu na ushughulikiaji wa pamoja wa changamoto ibuka duniani,” alisema Mudavadi.

Mudavadi alisema hayo alipowakilisha mipango ya maendeleo ya Kenya kwenye mkutano huo, huku akidokeza kuwa kuendelea kwa Korea kuwekeza katika miradi kama vile Konza Technopolis na taasisi iliyozinduliwa hivi karibuni ya Sayansi na Teknolojia (Kenya-AIST), kunaashiria kuimarika kwa ushirikiano katika ya Kenya na Korea katika maswala ya teknolojia, uvumbuzi na viwanda.

“Ushirikiano huu unaiweka Kenya kuwa kitovu cha uongezaji dhamani, uvumbuzi na ukuaji endelevu wa uchumi katika kanda hii,” alidokeza Mudavadi.

Share This Article