Zikisalia siku 10 pekee kabla ya kung’oa nanga kwa makala ya 23 ya fainali za Kombe la Dunia katika mataifa ya Mexico,Canada na Marekani,tuangazie mpira ujulikanao kama Trionda.
Mpira huu uliotengezwa na kampuni ya Adidas utatumika kwa mechi zote 104 za fainali za mwaka huu zitakazoshirikisha timu 48 kwa mara ya kwanza.
Mpira huu umetengezwa kwa teknolojia ya kisasa na unawezo kwa kunakili miguso yote na kutoa taarifa yote kwa haraka.
Trionda unafuata mipira ya awali ya Kombe la Dunia kama vile Telestar wa mwaka 1970, Tango uliotumika kuanzia mwaka 1978 hadi 88, na Jabulani uliotumika katika fainali za mwaka 2010 nchini Afrika Kusini.
Rangi tatu za Trionda za Nyekundu,Kijani na Samawati zinawakilisha mataifa ya Canada,Mexico na Marekani mtawalia.
Trionda umewekewa kifaa cha megahati 500, ambacho kinatoa taarifa nyingi kwa kila sekunde kwa maafisa wa kiufundi watakaosimamia mechi .
Kinyume na awali mpira wa Trionda, utaweza kuwasaidia Marefa na maafisa wa VAR kubaini kuhusu offsides na Handballs.
Mpira huo umetengezwa na kampuni ya Adiadas na unajumuisha vipande vinne vilivyounganishwa pamoja.
Fainali za Kombe la Dunia zitaandaliwa kati ya Juni 11 na Julai 19 mwaka huu.
Argentina ndio mabingwa watetezi huku Brazil iliwa timu iliyofanikiwa zaidi ikishiriki fainali zote 22 zilizopita na kutwaa ubingwa mara tano.