Timu ya taifa ya Kenya kwa wanawake wasiozidi umri wa miaka 17, itakabiliana na Afrika Kusini katika raundi ya tatu na ya mwisho kufuzu kwa Kombe la Dunia.
Junior Starlets walioibandua Uganda katika raundi ya pili kwa bao la ugenini watamenyana na Afrika Kusini, katika mkumbo wa kwanza wa raundi ya tatu kati ya Julai 3 na 5 ugenini,kabla ya mkondo wa pili kupigwa Nairobi wiki moja baadaye.
Afrika Kusini ilijikatia tiketi kwa raundi ya tatu kufuatia ushindi wa 2-0, dhidi ya Tanzania .
Mshindi wa jumla atafuzu kwa Kombe la Dunia baina ya Oktoba na Novemba, mwaka huu nchini Morocco.