Gor Mahia FC watatawazwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya, kwa mara ya 22 siku ya Jumapili ,baada ya mechi yao ya kufunga msimu dhidi ya Nairobi United FC katika uga wa Nyayo.
K’ogalo wametwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza tangu msimu wa mwaka 2023/2024,kabla ya kupokonywa taji na Police FC msimu jana.
Mechi zote za kufunga msimu zitachezwa sambamba kuanzia saa tisa alasiri.
Gor wanaongoza ligi ya Sportpesa kwa alama 69,pointi 5 zaidi ya AFC Leopards walio katika nafasi ya pili.
Ulinzi Stars,Mathare United na Kariobangi Sharks pia zitakuwa zikijaribu kuepuka kuwa timu ya mwisho kuenguliwa ligini.
Mechi za Ligi raundi ya 34
Gor Mahia FC vs Nairobi United FC
Kariobangi Sharks vs Sofapaka
AFC Leopards SC vs Bidco United FC
Mathare United FC vs Bandari FC
Murang’a Seal FC vs Mara Sugar FC
Police FC vs Kakamega Homeboyz
Posta Rangers vs Ulinzi Stars
Shabana FC vs KCB FC
Tusker FC vs APS Bomet FC