Kenya yaiparuza Namibia, yaingia raundi ya pili kufuzu Kombe la Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya kwa mabanati wasiozidi umri wa miaka 17 imeititiga Namibia magoli 5-0, katika marudio ya raundi ya kwanza kufuzu kwa Kombe la Dunia Jumamosi jioni katika uwanja wa Ulinzi .

Kenya imejikatia tiketi kwa raundi ya pili kwa ushindi wa jumla wa mabao 7-1, baada ya kushinda mkumbo wa kwanza 2-1, wiki jana mjini Windhoek,Namibia.

Harambee Starlets wanaofunzwa  na Mildred Cheche, watakutana na Uganda kwenye raundi ya pili baada ya Uganda kuwatimua Zimbabwe.

Share This Article