Watu watatu wafariki baada ya ndovu kusababisha ajali Uganda

Gari hilo lilikuwa limewabeba maafisa saba kutoka mamlaka ya kukusanya ushuru nchini Uganda (URA).

KBC Digital News
1 Min Read

Watu watatu wamefariki baada ya ndovu kusababisha ajali ya barabarani katika mbuga ya wanyamapori nchini Uganda.

Kulingana na Jeshi la Polisi la Uganda, watu wengine wanne walijeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea katika mbuga ya wanyama ya kitaifa ya Murchison Falls, kaskazini magharibi mwa taifa hilo.

Gari hilo lilikuwa limewabeba maafisa saba kutoka mamlaka ya kukusanya ushuru nchini Uganda (URA).

Mamlaka ya wanyamapori nchini Uganda, imewataka madereva kuwa waangalifu wanapotumia barabara ambazo hutumiwa na wanyama pia.

Share This Article