Uchunguzi waanzishwa kuhusu kifo cha Mkenya Australia

Tom Mathinji
1 Min Read
Kenya na Australia zaanzisha uchunguzi kuhusu cha Mkenya nchini Australia.

Serikali ya Kenya na ile ya Australia zimeanzisha uchunguzi wa pamoja kuhusu kifo cha Mkenya jijini Sidney, Australia.

Ukithibitisha kifo cha  Sheila Chebii siku ya Jumatatu, ubalozi wa Kenya wa Canberra, ulisema unashirikiana kwa karibu na maafisa wa nchi hiyo, kupata habari  kamili kuhusu tukio hilo kuambatana na taratibu za  sheria za taifa hilo.

Ubalozi huo ulidokeza kuwa unafahamu wasiwasi ulioibuliwa kufuatia kisa hicho, na likatoa wito kwa wananchi kuwa watulivu, kutoa fursa kwa uchunguzi.

“Ubalozi huu unawahimiza wananchi kutotoa habari za kupotosha, huku mamlaka husika zikiendelea na uchunguzi,” ilisema taarifa kutoka kwa ubalozi huo.

Aidha, iliongeza kuwa imejitolea kulinda maslahi ya Wakenya nchini Australia, New Zealand na mataifa ya visiwa vya Pacific, na litaendela kuwasiliana kupitia mifumo ifaayo.

Share This Article