Watu wawili zaidi waambukizwa Ebola nchini Uganda

Aidha, serikali imewaomba raia kuripoti mtu yeyote atakayeonyesha dalili za Ebola kwa maafisa wa afya.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wizara ya Afya nchini Uganda imetangaza visa viwili vipya vya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola na kufikisha idadi ya maambukizi kuwa tano kufikia sasa.

Kulingana na taarifa ya wizara hiyo, waathiriwa hao wawili ni wahudumu wa afya katika kituo kimoja cha afya cha kibinafsi jijini Kampala.

Watu wote waliotangamana na wagonjwa hao wawili wanatafutwa ili kuzuia msambao wa ugonjwa huo.

Aidha, serikali imewaomba raia kuripoti mtu yeyote atakayeonyesha dalili za Ebola kwa maafisa wa afya.

Share This Article